Job 6:14-20


14 a“Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,
hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.
15 bLakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,
ni kama vijito vya msimu,
ni kama vijito ambavyo hufurika
16 cwakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,
ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,
17 dlakini hukauka majira ya ukame,
na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.
18Misafara hugeuka kutoka njia zake;
hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia.
19 eMisafara ya Tema inatafuta maji,
wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri
hutazama kwa matarajio.
20 fWamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini;
wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia.
Copyright information for SwhNEN